Monday, August 27, 2012

BBC DIRA YA DUNIA KURUKA LEO KWENYE TV KWA MARA YA KWANZA



Saleem Kikeke

Matangazo ya televisheni ya Dira ya Dunia ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC leo yanaanza kuruka rasmi kupitia Star TV ya Tanzania na Qtv ya Kenya.

Wiki iliyopita kulifanyika uzinduzi wa matangazo hayo jijini Dar es Salaam.

Matangazo hayo ya Dira ya Dunia kwa upande wa radio ni maarufu zaidi pengine kuliko matangazo yote ya radio za kimataifa zinazotangaza Kiswahili duniani.

Kuingia kwenye matangazo ya runinga kwa BBC Swahili kunafungua ukurasa mpya wa matangazo ya aina hiyo ya Kiswahili nchini.

BBC Dira ya Dunia siku za usoni itakuwa ikishindana na matangazo mengine ya Kiswahili ya Al-Jazeera ambayo yapo kwenye mchakato wa kuanzishwa.

CHADEMA WAPIGWA MABOMU MOROGORO



 Huyu ni Ally Zona muuza magazeti wa Msamvu Morogoro akiwa hajitambui baada ya kutandikwa risasi na Polisi kuzuia maandamano ya chadema
Mtu mmoja anadaiwa kufa kwa kupigwa risasi Kichwani huku wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya kwa Risasi za moto baada ya Polisi kuwarushia Risaasi za moto na mabomu ya machozi waandamani wa Chadema mjini hapa.

Wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema
 Askari waliokuwa katika eneo la tukio kabla ya kuanza kwa maandamano hayo
 Moshi wa mabomu yaliolipuliwa kutawanya maandamano ya chadema leo mjini morogoro

 Gari  la chadema lililokuwa likiongoza maandamano hayo
Mmoja wa kiongozi wa chadema akiwa amekamatwa akiwa ndani ya gari la polisi 
 Wafuasi wa chadema wakiwa na maandamao hayo mjini morogoro

AKI APATA MTOTO WA KIKE

Nguli wa filamu nchini Nigeria Chinedu Ikedize alias AKI amefanikiwa kupata mtoto wa kike kutoka kwa mkewe Nneoma Hope Nwajah aliyejifungua siku kadhaa za nyuma nchini Nigeria.
Aki na mkewe huyo walifunga ndoa November 26 mwaka 2011 iliyofanyika nchini kwao na kuhudhuliwa na Celebrities kibao kutoka sehemu mbalimbali wakiwemo P-Square. Aki kwa sasa anaitwa baba akiwa na umri wa miaka 34.

SABABU 5 KWANINI LIGI KUU YA ENGLAND NDIO BORA DUNIANI




Inapewa sifa kuliko inavyostahili? Labda. Lakini kuna sababu kwanini English Premier League inaonekana kwa upana zaidi kama ligi bora kabisa ya ndani ya nchi duniani kote.

Huku ikiwa na miaka 20 tangu kuanza kwake, Premier league imekuwa chombo kilichobadilishwa namna soka inavyoangaliwa, mpaka inavyochezwa.

Premier league ilizaliwa mwaka 1992 kutokana na matamanio ya vilabu vikubwa vya England kupata faida kubwa kutokana na haki za matangazo ya Televison.

Ulikuwa ni muda ambao soka la England lilikuwa linatoka kwenye muda ambao ulikuwa ni giza la uhuni, ukosefu wa mashabiki viwanjani na ukosefu wa mvuto.

Huku kukiwa na uwepo wa fedha nyingi, utangazwaji na hamu ya kutaka kuiteka dunia, Premier league inaendelea kuitawala tasnia ya soka duniani leo hii.

Hizi ndio sababu 5  kwanini Premier League ndio ligi bora duniani.


WINGI WA UPINZANI WA VILABU VYA NDANI

 
England ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na vilabu vya juu, ambavyo vinatoa utajiri wa wingi wa upinzani wa vilabu vya ndani.

Kuna kipute cha upinzani cha London ya kaskazini, kipute cha upinzani wa mji Birmigham na vipute vingine kibao vya ndani ya nchi hiyo....OK, kati ya mechi hizi hakuna inayoweza kuifikia utamu wa kipute kati ya Real Madrid dhidi ya Barcelona, au Boca Juniors dhidi ya River Plate - lakini kikubwa zaidi kuna mechi mbili tu kwa msimu zinazohusisha upinzani mkubwa, tofauti na England ambapo kila wiki kuna uwezekano wa kuangalia mechi ya upinzani wa juu.

 MECHI KUTOKUTABIRIKA

 
Moja ya sababu kubwa nyingine inayoipa ubora ligi kuu ya England ni kutokutabirika kwa mechi.

Japokuwa ni ukweli kwamba ni vigumu kwa timu kama Southmpton kuwa mabingwa bila msaada wa matajiri wenye za kutupa kama akina Shekhe Mansour , lakini premier league bado inatoa level ya juu ya suhindani kutofautisha na ligi nyingine duniani.

Imekuwa kitu cha kawaida sana kuona Manchester United ikifungwa na timu ndogo au ikipata shida sana kupata japo sare. Tofauti na Spain ambapo inapocheza Barelona na Recreativo Huelva unajua leo Lionel Messi anatupia hat trick ngapi, lakini ni vigumu kufikiri hivyo inapocheza Chelsea na Reading au Manchester City na QPR.



Ikumbukwe moja ya mechi zilizosababisha Manchester United kukosa ubingwa kwenye dakika za mwisho ilikuwa dhidi ya timu iliyokuwa ikipambana kushuka daraja Wigan, - Ni vigumu kuona Real Madrid wanafungwa na timu inayoshika mkia kwenye la liga.

UPINZANI WA VILABU VIKUBWA

 
Mbali wa upinzani mkubwa timu zinazotoka sehemu moja: mfano Aston Villa vs Birmigham. Pia kuna wingi wa upinzani wa vilabu vikubwa.

England kuna utamu wa Mechi mbili za Manchester United dhidi ya Man City, Liverpool vs United, Arsenal vs Chelsea, Tottenham vs United, Arsenal vs Tottenham, United vs Chelsea,Tottenham vs City, Arsenal vs United, City vs ARsenal na nyingine kibao.

Mechi za namna hii ni vigumu kupata kwenye ligi nyinginezo duniani.


 USHINDANI

 
Moja ya hoja wanazotoa wapinzani wa Premier league ni ukosefu wa ushindani, hoja ambayo inakuja kutokana na ligi kuu ya England tangu uanzishwa kwake Manchester United imechukua ubingwa mara 12 kati ya 20.

Lakini hao hao United wamekuwa sio watawala wa ligi kuu ya England wamekuwa wakifanya vizuri sana kwenye mashindano ya kimataifa. Katika cha miaka mitano iliopita United wamecheza fainali 3 za champions league. Hii inaonyesha ni kiasi gani England inatoa bingwa sahihi.

Premier league pia imekuwa ikitoa nyingi kwenye mashindano ya kimataifa ambazo zimekuwa zikifanya vizuri.

Mwaka jana Manchester City ilikuwa ni klabu ya tano kushinda ubingwa wa EPL. Mabingwa watano tofauti kwenye kipindi cha miaka 20. Huu ni uwiano mzuri wa ushindani. Sasa Angalia ligi ya Spain, kwenye kipindi cha miaka 20 iliyopita imetoa mabingwa wanne, huku katika katika historia ya ligi hiyo tangu kuanzishwa kwake miaka 90 iliyopita imetoa mabingwa tisa tu.

MAFANIKIO YA ULAYA

 
Moja ya sababu kubwa ya kufanya mapinduzi ya kuileta Premier League ilikuwa ni kuleta upinzani mkubwa  ambao ungetosha kuwafanya kuitawala soka la bara la ulaya.

Ilichukua miaka kadhaa, lakini kwa sasa inaonekana wamefanikiwa vizuri sana.

Makombe manne kati ya 20 ya champions league yamechukuliwa na vilabu vya Premier League, matatu kati ya hayo ndani ya miaka 10 iliyopita. Fainali tano za champions league zilizopita zimekuwa zikihusisha vilabu vya England - United na Chelsea.

Kama, wengi wanavyosema kwamba Champions league ndio roho ya ubora wa soka, basi Premier league inastahili kuitwa ligi bora duniani.

By Aidan Seif Charlie

SERENGETI FIESTA BONANZA YATINGISHA JIJI LA MAHABA TANGA

.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group, Joseph Kusaga usiku huu mara baada ya kuwataja washindi waliojishindia piki piki mara baada ya kuchezeshwa bahati nasibu,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea,pichani kati ni Afisa Mahusiano wa Clouds Media Group, Simon Simalenga.
Steve Nyerere & Shilole kazi ipo.......
Shilole & JB
FA & Linah ni Yalait au kunamengine??? LOL!
Wema,Aunt & Shilole....Mmmmmmmh!!! Kazi ipo
Rachael.....

CMB Prezzo 4rom Kenya Bhaaasss!
Mwana FA ndani.....
Shetta wa Darstamina kwa steji akidanganywadanganywa.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nuru akitumbuiza jukwaani usiku huu na shabiki wake mbele ya wakazi wa jiji la Tanga wanaondelea kutiririka ndani ya uwanja wa Mkwakwani ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
.
Dj Zero kutoka Clouds FM akikamua.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Tanga wakifuatilia kwa makini makamuzi ya Fiesta usiku huu.


Mambo ya Fiesta Serengeti 2012 ndani ya Jiji La Tanga.

 Show Love.



 Mtangazaji Millard Ayo akifanya mahojiano na Sam Baruti.
 
 Mwanadada Loveness Love akiongea machache na wakazi wa Tanga.

 Kwenye moja na mbili toka ndani ya viwanja vya Tangamano.
 
 

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine