UONGOZI wa klabu ya Azam umesema kama Simba na Yanga wanaona kuna maslahi wanayopoteza wakitumia Uwanja wa Chamazi, basi wanaweza kuondoka na kutafuta viwanja vingine.
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Said Mohammed amesema wanasimamia kwenye maadili na kwamba wamekataa kuweka mabango ya kampuni ya bia ambao ni wadhamini wa Yanga na Simba kwa sababu za kibiashara, hivyo Simba na Yanga wanaweza kufanya uamuzi.
Simba na Yanga wanaweza kutumia uwanja wetu, lakini jambo la mabango linatakiwa kuangaliwa kwa umakini wa hali ya juu, kwa sababu hata kwenye viwanja vingine duniani ipo.
Vodacom walipotaka kuweka ya kwao walikuja tukazungumza, lakini ieleweke kuwa sisi tuna maadili na miiko yetu. Hivyo ambao wanaotumia uwanja wetu wanatakiwa kuyafuata, wakishindwa wanaweza kuondoka na kwenda kutafuta viwanja vingine,” alisisitiza Mohammed.
Hivi karibuni kuliibuka hoja juu ya kuzuiliwa kwa mabango ya kuitangaza kampuni ya bia ambayo ni wadhamini wa Simba na Yanga.
Hivi karibuni kuliibuka hoja juu ya kuzuiliwa kwa mabango ya kuitangaza kampuni ya bia ambayo ni wadhamini wa Simba na Yanga.
0 comments:
Post a Comment