Baada ya madaktari kutangaza kuanza mgomo jumatano march 7 2012, Waziri mkuu Mizengo Pinda akizungumza kwa upole amesema “bado napata imani kwamba huenda busara zikatumika kwa madaktari hao na wakajirudi, na wakaachana na mgomo kwa sababu napata tabu sana kama kweli wanaweza kuendelea kusema wacha vile vitoto vife, vibibi vife, inaniumiza sana kichwa”
Amesema “tutaamka asubuhi na kukuta hali ndio hiyo hiyo basi itabidi serikali iangalie tufanye nini kwenye mazingira hayo”
hata hivyo waziri mkuu amezungumzia ishu ya madaktari hao kumuamuru kutekeleza wanachotaka ndani ya saa 72 kwa kusema “hoja hapa ni ile kufanya kwamba ni sharti kabla ya majadiliano, ningeelewa kama ningeulizwa muheshimiwa lile jingine mnakwenda nalo vipi? ila shida ni ile unanipa saa 72 kwa sababu umeshika mpini mwingine kashika makali, inanipa tabu sana kwamba hata kesho mtafanya hivyo, na hata kesho kutwa na siku nyingine mtaendelea hivyo hivyo ndio maana nasema hapana, hili jambo lilielezwa vizuri na process zake zinaendelea yani lilikua swala la kutaka kujua tu limefikia wapi”
Upande wa Madaktari umesisitiza kwamba wanachohitaji ni viongozi wakuu wa wizara ya afya kuondolewa kwenye nafasi hizo moja kwa moja, akiwemo Katibu mkuu na waziri wake.
0 comments:
Post a Comment