Milovan Cirkovic, kocha mkuu wa Simba
Kocha
mkuu wa Simba Milovan Cirkovic, amemkabidhi majukumu beki wake Shomari
Kapombe ili kuhakikisha anakula sahani moja na mshambuliaji wa Yanga
Saidi Bahanuzi katika mechi ya kesho ya ligi kuu ya Vodacom baina ya
timu hizo kwenye dimba la Taifa.
Milovan
alisema amempa majukumu hayo Kapombe kutokana na aina ya uchezaji
anaocheza hasa wa kutumia akili pamoja na nguvu na haswa ikizingatiwa
kuwa anajua namna ya kukaba na ni mwenye kujua nini anafanya ili
asilete madhara langoni mwake anapokuwa uwanjani kwa muda wote wa
mchezo.
Mserbia
huyo alisema anaamini Bahanuzi ni mmoja wa washambuliaji mahiri na
wenye kutumia akili na nguvu hivyo kutomuwekea ulinzi imara anaweza
kufanya kitu mbaya kwa timu yao.
“Namuamini
Kapombe na anaweza kuwa mtu muhimu katika ulinzi katika mechi ya
keshokutwa hivyo wanasimba wanahitaji kumpa msaada kwa muda wote wa
mchezo.
Aidha
kocha huyo amewataka wana Simba kuwa watulivu kwanai ana uhakika wa
kushinda katika mechi hiyo kutokana na maandalizi ya uhakika aliyofanya.
0 comments:
Post a Comment