Meneja
wa huduma za jamii wa Vodacom Foundation, Mwamvua Mlangwa akikabidhi
mfano wa hundi ya fedha kiasi cha shilingi Milioni 20, kwa Mkurugenzi wa
kituo cha Tanzania Mitindo House, Khadija Mwanamboka, Kwa ajili ya
kuanzisha chuo cha mafunzo ya Mitindo kwa Watoto yatima.
---
Dar es Salaam, Zaidi ya watoto yatima 50 waishio katika
mazingira magumu watapata mafunzo ya ubunifu wa mavazi. Hii inafuatia
kuanzikwa kwa kwa kituo cha ubunifu wa mavazi, (Mitindo House)
kitakachokuwa chini ya Mwanamitindo maarufu, Khadija Mwanamboka.
Kituo hicho kitatoa mafunzo ya ushonaji, ubunifu wa mavazi, na
utengenezaji wa vito mbalimbali kimefadhiliwa na mfuko wa huduma za
jamii wa Vodacom (Vodacom Foundation)
Akizungumza baada ya kupokea mfano wa hundi ya shilingi Milioni
Ishirini, Mkurugenzi wa kituo hicho, Hadija Mwanamboka, amesema kuwa
lengo lao ni kuwawezesha watoto yatima waishio katika mazingira magumu
na wasio na elimu kuweza kujitegemea kwa kujiajiri wenyewe kutokana na
ujuzi watakao upata.
“Tutatoa mafunzo kwa watoto wanaoishi katika vituo mbalimbali vya
kulelea watoto yatima, yatakayo wawezesha kupata fursa ya kuonyesha
vipaji vyao katika majukwaa ya sanaa na baadae kuwawezesha kujiajiri wao
wenywe.”
“Mafunzo haya yatatolewa kwa mwaka mzima, wanafunzi ishirini na
tano watapata mafunzo ya ushonaji na ubunifu wa mavazi na wengine 25
watapata mafuzno ya uchongaji wa vito mbalimbali na uchoraji,” alisema
Hadija.
Kwa upande wake, Meneja wa Huduma za jamii wa Vodacom Foundation,
Mwamvua Mlangwa amesema kuwa Vodacom Foundation imedhamiria kuboresha
maisha ya jamii ya watanzania wanaoishi katika mazingira magumu.
“Vodacom Foundation itaendelea kuwaunga mkono watanzania hususani
wale wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwasaidia kujenga maisha yao
na kusaidia kukua kwa uchumi wa nchi kupitia mipango mbalimbali
tuliyonayo katika kitengo chetu,” alisema Mlangwa.
Kuhusu Vodacom Tanzania:
Kampuni ya Vodacom Tanzania Limited ina dhamira ya dhati ya
kushirikiana na jamii katika shughuli za maendeleo kupitia taasisi yake
ya Vodacom Foundation. Vodacom Foundation ina nguzo kuu tatu: Afya,
Elimu na Ustawi wa Jamii. Hadi sasa taasisi hiyo imechangia zaidi ya
miradi 120 ya kijamii nchini. Aidha, imeshinda tuzo mbalimbali za
kitaifa na za kimataifa katika nyanja ya Uwajibikaji wa Mashirika kwa
Jamii. Hizi ni pamoja na East African CSR Awards na Diversion and
Inclusion Award ambayo hutolewa na kampuni mama ya Vodafone .
Vodacom Tanzania Limited ni kampuni ya simu za mikononi inayoongoza
Tanzania inayotumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano. Vodacom
Tanzania ni kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty) Limited, South Afritca,
ambayo pia ni kampuni tanzu ya Vodafone Group UK. Vodacom Group (Pty)
Limited inamiliki hisa ailimia 65 Vodacom Tanzania na asilimia 35
zilizobaki zinammilikiwa na Mirambo Ltd.
Vodacom Tanzania imetangazwa kuwa Super Brand (Chapa Bora Zaidi) kwa miaka mitatu mfululizo, kutoka 2009 -2011.
CHANZO CHA HABRI: www.globalpublishers.info
0 comments:
Post a Comment