Monday, February 18, 2013

GHOROFA DAR LAANGUKA, LAUA

   Jengo hilo la ghorofa likiwa limeanguka.
Vikosi vya Zimamoto na Ukoaji vikiwa katika harakati za kuokoa waliofukiwa na kifusi cha jengo.
Mmoja wa aliyeokolewa ambaye alitambulika kwa jina moja la Clementina akisaidiwa na baadhi ya askari.
...Akiingizwa katika gari la wagonjwa tayari kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala.
...Umati ukiwa eneo la tukio.
WAKAZI wa Kijitonyama B Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam jana waliingiwa na simanzi kubwa baada ya jengo la ghorafa tatu ambalo lilikuwa halijakamilika kuangua na kusababisha kifo cha mtoto wa miaka tisa.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa majirani zinasema kuwa jengo hilo lilikuwa halina sifa ya kukaa mtu maana lilishapigwa marufuku kuendelea kujengwa.
Waandishi wetu walipofika eneo la tukio walishuhudia watu wakihangaika kutafuta waliokuwa wameangukiwa na jengo hilo.

(Picha/Habari: Haruni Sanchawa na Makongoro Oging)
CHANZO CHA HABARI : www.globalpublishers.info

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine