Mpaka sasa ameshatoa ajira kwa vijana wenzake sita na bado anasema kuna nafasi za ajira kwa vijana ambao wanadhani wanavigezo vya kufanya kazi ya utengenezaji movie wakiwa ni wataalamu wa vitu mbalimbali.
Kampuni hiyo itakua pia inahusika na kuvifanyia kazi vipaji vya waigizaji wapya na kuwapa nafasi ya kuonekana wakiwa tayari na mikataba mizuri chini ya usimamizi wa Wema Sepetu likiwa pia ni moja ya malengo yake kwenye hiyo kampuni.
Mama mzazi wa Wema anasema anamshukuru sana Marehemu Kanumba manake ndio alimshawishi ampe Wema ruhusa ya kuingia kwenye uigizaji mpaka kutimiza ndoto kama hii.
Huyu
ni mama mzazi wa Wema katika ofisi ya Wema ambayo ipo ghorofa ya kwanza
kwenye nyumba ambayo ipo Kinondoni Dar es salaam karibu na Biashara
Complex.
.
0 comments:
Post a Comment