Wednesday, July 20, 2011

TWANGA PEPETA YABOMOLEWA TENA.

BENDI ya Muziki wa Dansi ya Extra Bongo ya jijini Dar es Salaam ‘Watoto wa Bongo’, imezidi kujiimarisha baada ya kumnyakua mnenguaji mahiri hapa nchini, Aisha Madinda kutoka kwa wapinzani wakubwa wa bendi hiyo, African Stars ‘Twanga Pepeta’.

Akimtambulisha mnenguaji huyo leo katika ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo Makumbusho jijini, kiongozi wa bendi hiyo, Kamaladee Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’ alisema kuwa, mnenguaji huyo ametua katika bendi hiyo kuimarisha safu yao ya unenguaji.



Baada ya utambulisho huo, Aisha aliwaambia waandishi wa habari kuwa, ametua katika bendi hiyo ili afanye kazi na amewataka mashabiki wake wasubiri vitu vyake vipya.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine