Saturday, October 15, 2011

WEMA NA MAMA MKWE HAWAIVI.



Na ERIC PIUS

Kuna madai kuwa mchumba wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, Wema Sepetu na mama mkwe wake hawaivi chungu kimoja kutokana na mama huyo kutomkubali, Risasi Jumamosi linashuka kijasiri.

Habari zinadai kuwa mama huyo amekuwa hamkubali Wema kutokana na tabia zake achilia mbali skendo za mara kwa mara kwenye vyombo vya habari.

“Unajua Wema ana skendo kibao, nyingine zinaandikwa, nyingine ‘jukwaju’ ndiyo maana mama mkwe wake hamkubali hata kidogo,” kilisema chanzo.

Madai haya yalilifikisha Risasi Jumamosi kwenye kumtafuta Diamond kwa njia ya simu ambapo alipopatikana alifunguka:
“Hizo habari mimi mwenyewe nazisikia sana mtaani kuwa mama yangu eti anamchukia Wema, hakuna kitu kama hicho, hizo ni redio mbao tu na sijui watu wanakuwa na maana gani? Mimi nashangaa sana, kwa sababu Wema tunakaa nyumba moja na mimi pamoja na mama, sasa kama angekuwa anachukiwa si angetimuliwa nyumbani jamani!

“Unajua watu wasiwe wanaongea vitu ambavyo hawavijui bali wawe na uhakika ‘bhana’ hebu watuache, kama hawamtaki Wema wao mama ameshamkubali watake wasitake,” alisema Diamond
.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine