Thursday, December 8, 2011

AKUTWA AKIWA AMEKUFA HOTELINI PAMOJA NA MZIGO WA MADAWA YA KULEVYA.


Mtu mmoja aliyefanhamika kwa jina la  Bushaga Masalai ambaye ni mkazi wa jijini Dar es salaam ambaye ni mfanyabiashara kati ya miji ya Mbeya,Dar na nchi jirani ya Zambia amekutwa amefariki kwenye hoteli inayofahamika kwa jina la High Class iliyoko kwenye mji wa Tunduma jijini Mbeya.Chanzo cha kifo chake hakijafahamika na marehemu huyo alikutwa na kete 60 za madawa ya kulevya,kifo hicho kilifahamika baada ya wahudumu wa hoteli hiyo
kugonga kwenye mlango wa chumba hicho mnamo tarehe 3 mwezi huu kwa minajiri ya kufanya usafi lakini hawakupata jibu kutoka ndani na ndipo walipolazimika kutoa taarifa polisi ambao walifika baadae na kuvunja mlango wa chumba hiko na kumkuta mtu huyo akiwa amefariki,madawa hayp yanatarajiwa kufikishwa kwa mkemia mkuu kwa ajili ya uchunguzi.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine