Thursday, December 15, 2011

Kumbe Badra ni mjamzito




KUMBE msanii anayetikisa mkia kunako Tasnia ya Filamu Bongo, Latifa Shaaban Idabu ‘Badra’ (pichani) ana ujauzito wa miezi mitatu, Amani limeibumburua.
Habari za msanii huyo kunasa kichanga kitarajiwa, zilivujishwa na mmoja wa rafiki zake wa karibu ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini.
“Nakupa umbeya lakini usinitaje, Badra ana ujauzito, tena wa miezi mitatu ila anafanya siri ili bwana ‘ake anayejulikana kwao asijue maana si yake,” alisema.
Juzikati, wakati paparazi wa habarizaudaku.com akiwa kazini, maeneo ya Magomeni, Dar, alimuona msanii huyo  akiwa na wasanii wenzake wakirekodi sinema mpya iitwayo I Must Die, akaona ndiyo nafasi ya kuthibitisha ukweli wa  habari hiyo, lakini akaambulia matusi.

“Unaulizia ujauzito wangu wewe kama nani? Wee fa** (tusi) nini? Achana na maisha yangu, hayakuhusu! Niwe na mimba, nisiwe nayo si kazi yako kujua,” alikuja juu Badra.

Hata hivyo, muonekano wake ulionesha dhahiri kuwa amemeza ‘kijusi’ tumboni, kwani kwa mbali kitumbo kilionekana.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine