
RB namba KLR/RB/ 5969/2011 imemtia korokoroni mwanamuziki wa Msondo Music Band, Hassan Moshi ‘TX Junior’ (pichani) kwa shitaka la kutishia kuua kwa maneno.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda, mlalamikaji wa kesi hiyo ni mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Doreen.
Ilidaiwa kuwa wiki mbili zilizopita, TX Junior alikwenda nyumbani kwa Doreen usiku na kumfanyia fujo iliyoambatana na kipigo baada ya kusikia kuwa ana kidume kingine ‘anachombonji’ nacho.
Blog ya Habarizaudaku.co.cc ilipewa nyenzo za kuzungumza na Doreen ambapo alipopatikana alikiri kujuana kimapenzi na TX Junior kwa siku za nyuma hivyo kuonesha kushangaa fujo za jamaa huyo ilihali ana mwanamke mwingine.
Kwa mujibu wa Doreen, mbali na kipigo, pia alimtishia kumuua na kwa kuwa bado anapenda maisha, alikwenda kumfungulia kesi katika Kituo cha Polisi cha Kilwa Road, Dar es Salaam ambapo jamaa alitiwa mbaroni na kukaa nyuma ya nondo kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa kwa dhamana.
Habarizaudaku.co.cc ilivyotaka kusikia neno la TX Junior, hakuwa tayari kwa madai kwamba tayari ishu iko mikononi mwa polisi na paparazi wetu alipotimba kituoni hapo alithibitishiwa kuwepo kwa kesi hiyo.
0 comments:
Post a Comment