Afisa mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania Bi. Dangio Kaniki akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kutangaza washindi wa promosheni ya Mkali nani ambapo washindi wa siku hujinyakulia kitita cha shilingi milioni moja na washindi wa wiki hujinyakulia kitita cha shilingi milioni tatu,kutoka kushoto ni Afisa Uhusiano wa kampuni ya Airtel Bi. Jane Matinde akishuhudia tukio hilo lililofanyika makao makuu ya kampuni hiyo eneo la morocco jijini Dar-es-Salaam.
Washindi 7 wa kila siku na mshindi wa wiki atangazwa 29, March 2012 Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo imewatangaza washindi wa wiki hii ya promosheni ya nani Mkali pesa taslimu ambapo washindi wa kila siku watakabidhiwa shilingi milioni moja kila mmoja na mshindi wa wiki ataondoka na shilingi milioni tatu. Washindi hao wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali Tanzania ikiwepo Arusha, Zanzibar, Dar es Salaam, Nzega - Tabora na Manyara
Akiongea wakati wa kukabithi zawadi hizo Afisa uhusiano wa Airtel Dangio Kaniki alisema" Airtel inawapa nafasi nyingine watanzania kushiriki na Kushinda fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 200,kwa washindi 110 watakaopatikana kila siku, kila wiki na kila mwezi katika promosheni yetu kabambe ya Nani Mkali. Na leo napenda kuchukua fulsa hii kuwatangaza washindi wa wiki hii ambao ni;
KAANAEL LEMLE KANUYA WA ARUSHA
(50) 1,000,000.00
(50) 1,000,000.00
RAKESH MANSUR DEYAL WA ZANZIBAR
(34) 1,000,000.00
(34) 1,000,000.00
NAPEGWA DAVID MONGO WA DSM
(58) 1,000,000.00
(58) 1,000,000.00
MARIAM WAZIRI HAMISI WA DSM
(32) 1,000,000.00
(32) 1,000,000.00
GUVANTRAI SACHDEV SHANTILAL WA ARUSHA
(54) 1,000,000.00
(54) 1,000,000.00
YUSUPH NOHAI ANNAI WA MANYARA
(35) 1,000,000.00
(35) 1,000,000.00
YUSUPH MATHIAS MANONI WA NZEGA-TABORA
(25) 3,000,000.00
(25) 3,000,000.00
0 comments:
Post a Comment