Star wa zamani wa lebo ya MUDER INC mwimbaji ASHANTI amekubali kwamba mastaa wengi duniani wanauza muziki kutokana na skendo zao kwa sababu binadamu wa sasa wanafatilia sana maisha ya mtu kuliko kazi anayofanya.
Kwenye interview na HOT 107, Ashanti ambae ana single mpya na Busta Rymes sasa hivi ya ‘the woman you love’ amesema hiyo ni sehemu ya biashara kwa sasa na ni lazima staa yeyote akubaliane nayo au aitarajie.
Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na NELLY, Ashanti amekwepa hilo swali na kuzuga kwa kucheka na kutotaka kuliongelea kabisa na kufanya watu waamini kwamba jamaa wamemwagana kwa sababu kwenye uhusiano wao wamekua wakiachana na kurudiana mara kadhaa.
Alipoulizwa huwa anachukua muda gani kukutana kimapenzi na mpenzi mpya, Ashanti amesema huwa inachukua mwaka mzima hataki iwe rahisi na katika aina ya mwanaume anaemtaka kwenye maisha yake ya kimapenzi ni lazima awe na lips nzuri, mdomo mzuri na anukie vizuri pia, hivyo ni moja kati ya vigezo.
0 comments:
Post a Comment