Kufungwa kwa dirisha Hilo kunamaanisha kuwa mchezaji aliyekuwa anatarajiwa kuihama timu Yake Dwight Howard ataendelea kubaki na Orlando Magic hadi mwisho wa msimu huu ambapo mkataba wake utakuwa unakamilika.
Taarifa toka kwa wawakilishi wa Howard zinasema kuwa mchezaji huyo ameeleza dhamira yake ya kutaka kuongeza mkataba wake kwenye timu hiyo japo wengi wanaamini kuwa Orlando Magic itampoteza mchezaji huyu kwani anaona kubakia kwenye timu hiyo kutamzuia kupata nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi ya NBA.
Hata hivyo tarehe hiyo ya mwisho ya mabadilishano ya wachezaji imeshuhudia Mtanzania anayecheza kwenye ligi hiyo akibadilisha timu kwa mara ya tatu, Hasheem Thabeet amehamishwa kwenye timu ya Portland Trail Blazers akitokea kwenye timu ya Houston Rockets .
0 comments:
Post a Comment