MAFISANGO NA SUNZU WAZIDI KUUIMARISHA UONGOZI WA SIMBA KILELENI - AZAM NAO WASHIKA NAFASI YA PILI.
Magoli yaliyofungwa na wachezaji wa kigeni kiungo wa wa Rwanda, Patrick Mutesa Mafisango dakika ya 18 na mshambuliaji wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. dakika ya 74, jioni ya leo kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro yameiwezesha Simba SC kukalia kwa madaha- kwa kujinafasi kiti cha uongozi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuibwaga Mtibwa Sugar 2-1.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Hussein Omar Javu aliifungia Mtibwa bao lililokuwa la kusawazisha dakika ya 52, ambalo mwisho wa mchezo lilikuwa la kufutia machozi- kufuatia Sunzu kutupia la ushindi kwa Simba.
0 comments:
Post a Comment