Friday, April 6, 2012

HAYA NDIO MATUMIZI YA UWOYA KWA SIKU



Irene Uwoya
WAKATI Watanzania wengi wanalalamikia ugumu wa maisha, hali ni tofauti kwa gwiji la filamu za Swahiliwood, Irene Uwoya, kwani yeye bajeti yake kwa siku ni zaidi ya mshahara wa mwezi wa watu wengi.

Habari zinasema kuwa katika suala la usafiri tu amekuwa akitumia gari la kifahari la kukodi, Range Rover, anayolipia Sh 450,000 kwa siku.

Mwanadada huyu ambaye mara nyingi filamu zake ni moja kati ya filamu ambazo hufanya vizuri sokoni, anaishi Kijitonyama katika moja ya nyumba yenye aliyopanga baada ya kuondoka kwao Mbezi.

Inasemekana kuwa Irene hapendi kutumia aina ya gari ambayo hata wasanii wengine wanaweza kutumia.

Lakini sasa imeelezwa ameachana na Range hiyo na amekodi Hammer ambayo kila baada ya siku nne anailipia Sh 4 milioni.

Mwanaspoti iliongea na mmiliki wa magari hayo na kuthibitisha kulipwa fedha hizo na Uwoya. Hata hivyo mmiliki huyo hakupenda kutajwa jina gazetini.

1 comments:

mangala phg said...

oya mbona habari inaishia njian

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine