Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki (Cecafa) limesema mashindano ya Kombe la Kagame mwaka huu yatakayofanyika jijini Dar es Salaam, yatagharimu dola 600,000 (sawa na Sh944 milioni).
Mwaka jana mashindano hayo yalidhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania TBL kupitia bia yake ya Castle kwa Sh300 milioni.
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alisema hayo wakati akifafanua bajeti ya mwaka huu ya mashindano hayo.
Akijibu
maswali aliyoulizwa na gazeti la East African Business Week, Musonye
alisema kwa asilimia kubwa, maandalizi ya mashindano hayo
yamekamilika."Hivi sasa tunasubiri timu kuthibitisha ushiriki wao ili
tuweze kupanga ratiba ya timu 12 zizotarajia kushiriki mwaka huu,"
alisema Musonye.
Musonye
aliwataka mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano
hayo yatakayofanyika Tanzania kwa mara ya tatu mfululizo, ambapo pia
yataonyeshwa katika kituo cha televisheni cha Super Sport.
Mashindano hayo yamekuwa yakidhaminiwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame tangu mwaka 2002. Kabla ya udhamini wa Kagame, mashindano yakijulikana kama Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati na yalianzishwa mwaka 1974.
Mashindano hayo yamekuwa yakidhaminiwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame tangu mwaka 2002. Kabla ya udhamini wa Kagame, mashindano yakijulikana kama Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati na yalianzishwa mwaka 1974.
Musonye
alisema mashindano hayo yanafanyika tena Tanzania kwa sababu ya
mafanikio yaliyopatikana katika mashindano ya Kombe la Chalenji na
Kombe la Kagame mwaka jana.Pia uhakikia wa udhamini ndiyo uliopelekea
mashindano hayo kufanyika tena Dar es Salaam, alisema zaidi Musonye.
Mwaka
jana mashindano hayo yalitakiwa kufanyika Zanzibar, lakini kwa sababu
ya ukata yakahamishiwa Sudan ambayo nayo ilishindwa kuwa mwenyeji wka
sababu ya matatizo ya kisiasa.
Hivyo
Cecafa iliamua mashindano hayo yafanyike jijini Dar es Salaam, ambapo
yalikuwa na mafanikio kwa sababu mapato ya viingilio yaliyopatikana
kwenye mechi za mashindano hayo yalikuwa sh 1.2 bilioni (dola
763,358).
Mashindano hayo ya Kagame yalikuwa na mvuto zaidi kuanzia hatua za robo fainali katika mechi tofauti zilizocheza timu za Simba na Yanga.
Mashindano hayo ya Kagame yalikuwa na mvuto zaidi kuanzia hatua za robo fainali katika mechi tofauti zilizocheza timu za Simba na Yanga.
Mashabiki
wa soka wa Afrika Mashariki walijikuta wakiacha kuangalia mechi za
Ligi Kuu ya England na kufuatilia mechi za mashindano ya Kombe la
Kagame mwaka jana hasa hasa kuanzia hatua ya robo.
Mwaka
jana timu 13 zilishiriki, ambazo ni Ulinzi (Kenya), Ports (Djibouti),
St George (Ethiopia), El Merreikh (Sudan), Red Sea (Eritrea), Elman
(Somalia), APR na Etincelles (Rwanda), Bunamwaya (Uganda), Vital'O
(Burundi) na wenyeji Simba na Yanga za Tanzania.
Mabingwa
watetezi wa michunao hiyo ni Yanga iliyoifunga Simba bao 1-0 katika
mechi ya fainali, shukrani kwa bao pekee la dakika za majeruhi kutoka
kwa mshambuliaji Ghana, Kenneth Asamoah.
0 comments:
Post a Comment