Taarifa zisizo rasmi na za kutoka
ndani kabisa ya kamati ya uchaguzi wa Yanga, zinasema aliyekuwa
mwenyekiti wa baraza la michezo nchini (BMT) Kanali Iddi Kipingu
anatarajia kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti wa klabu ya Yanga muda
wowote kutoka sasa.
Kipingu ambaye ni mdau mkubwa michezo nchini, akiwa ni mmoja ya watu waliochangia upatikanaji wa vipaji vya wachezaji wengi kama Juma Kaseja, Boniface Pawasa na wengine wengi wakati akiwa mkuu wa wa shule ya Makongo, anatarajiwa kuchukua fomu ndani ya kipindi cha masaa 72 kutoka kutoka sasa.
Kwa maana hiyo sasa Kipingu atakuwa akichuana na mfanyabiashara maarufu ambaye ameshaidhamini Yanga Yusuph Manji ambaye nae tayari ameshachukua fomu rasmi ya kugombea ubosi wa klabu bingwa ya afrika mashariki na kati.

chanzo cha habari: www.shaffihdauda.com
0 comments:
Post a Comment