Bendi dansi ya FM maarufu kama wazee WANGWASUMA pamoja na msanii wa vichekesho MPOKI watatoa burudani ya anina yake katika shindano la kumsaka malkia wa kitongoji cha Kigamboni City 2012' litakalofanyika Juni 15 mwaka huu katika ukumbi wa Navy Beach ulioko huko Kigamboni hapa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
jana jijini, Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu, bendi ya FM
inafahamika kwa kutoa burudani nzuri kwa mashabiki wa muziki wa dansi
nchini .
Kuhusiana
na msanii MPOKI, SOMOE amesema kuwa mchekeshaji huyo ambaye pia ni
mkazi wa KIGAMBONI amekuwa ni kati ya waburudishaji katika sanaa ya
uchekeshaji na kupendwa na watu wa rika zote hivyo mashabiki wa urembo
wataweza kupata burudani ya uhakika .
Mratibu huyo kutoka kampuni ya K& L, alisema kuwa Jumla
ya warembo 15 wanaendelea kujifua katika kambi ya mazoezi chini ya
mwalimu wao miss TEMEKE HAWA ISMAIL ambaye anashirikiana na mshiriki wa
miss TANZANIA mwaka jana BLESSING NGOWI.
Amewataja
warembo hao kuwa ni pamoja na CAROLYNE DANDU,FATINA FRANSIS,EDDA
SLYVESTER,AISHA MUSSA,ROSEMARY PETER,DOREEN KWEKA,CAROLINE PETER,AGNES
GOODLUCK,SOPHIA MARTINE,ROSEMARY DEOGRATIUS,BEATRICE BONIFACE,JULIETH
PHILIP na KHADIJA KOMBO.
"Kigamboni ni zaidi ya kitongoji, tunaamini shindano letu litakuwa na mvuto na hadhi ya kipekee kama eneo lake lilivyo," aliongeza.
Alisema kuwa warembo watakaofanya vizuri watapata nafasi ya kuwakilisha kitongoji hicho katika mashindano ya kanda ambayo yatafanyika baadaye mwaka huu.
Aliwataja wadhamini ambao tayari wamethibitisha kudhamini shindano hilo ni pamoja na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's, Dodoma Wine na NSSF,Hope country Motel,Norbro’s Collections,Screen masters,Global Publishers.
Salha
Israel kutoka Kanda ya Ilala ndiye mrembo anayeshikilia taji la taifa
ambapo mwaka huu ratiba ya mashindano hayo imebadilika.
0 comments:
Post a Comment