Saleem Kikeke |
Matangazo
ya televisheni ya Dira ya Dunia ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC leo
yanaanza kuruka rasmi kupitia Star TV ya Tanzania na Qtv ya Kenya.
Wiki iliyopita kulifanyika uzinduzi wa matangazo hayo jijini Dar es Salaam.
Matangazo
hayo ya Dira ya Dunia kwa upande wa radio ni maarufu zaidi pengine
kuliko matangazo yote ya radio za kimataifa zinazotangaza Kiswahili
duniani.
Kuingia kwenye matangazo ya runinga kwa BBC Swahili kunafungua ukurasa mpya wa matangazo ya aina hiyo ya Kiswahili nchini.
BBC
Dira ya Dunia siku za usoni itakuwa ikishindana na matangazo mengine
ya Kiswahili ya Al-Jazeera ambayo yapo kwenye mchakato wa kuanzishwa.
0 comments:
Post a Comment