Mahitaji
- Tambi (Spaghetti)
- Nyama ya kusaga
- Kitunguu maji
- Nyanya ya kopo
- Kitunguu swaum
- Tangawizi
- Carrot
- Hoho
- Lemon
- Chumvi
- Curry powder
- Mafuta
- Fersh coriander
Matayarisho
Katakata vitunguu maji, carrot, hoho, kisha weka pembeni.
Saga vitunguu swaum na tangawizi pamoja kisha weka pembeni. Baada ya
hapo injika sufuria jikoni, tia mafuta. Yakisha pata moto tia vitunguu
maji kaanga mpaka vigeuke rangi ya kahawia kisha tia kitunguu swaum na
tangawizi.baada ya hapo tia nyanya ya kopo na iache ichemke mpaka iive.
Baada ya nyanya kuiva tia curry powder na chumvi. Geuza mpaka
mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia nyama ya kusaga na uiache
ichemke mpaka iive.Baada ya nyama kuiva tia Corrot na hoho na uzipike
kwa muda wa dakika 2.Na baada ya hapo mboga itakuwa imeivaa, iipue na
katia fresh coriander. Baada ya hapo injika sufuria yenye maji jikoni.
Yaache yachemke na kisha tia chumvi na mafuta ya mzaituni (olive oil) na
tambi. Acha zichemke mpaka ziive kisha zichuuje maji na chujio na baada
ya hapo zitakuwa tayari kuseviwa na nyama.
0 comments:
Post a Comment