ALIYEKUWA Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu,
ameshinda kesi iliyokuwa inamkabili baada ya kuonekana ushahidi
uliotolewa na upande wa walalamikaji kutojitosheleza.
Akisoma hukumu hiyo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Hakimu Ilvine Mugeta, alisema baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili amebaini kuwa Profesa Mahalu na aliyekuwa Mkuu wa Fedha na Utawala katika ubalozi huo, Grace Martin, hawana hatia na hivyo kuwaachia huru.

PROF. MAHALU MARA BAADA YA HUKUMU KUSOMWA NA KUSHINDA KESI ILIOKUWA IKIMKABILI HABARI,PICHA KWA HISANI YA MICHUZI BLOG.
Hakimu Mugeta alisema kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa walalamikaji unajichanganya na kuonekana wazi kuwa tuhuma zilizokuwa zinamkabili Profesa Mahalu si za kweli.
0 comments:
Post a Comment