Wednesday, August 8, 2012

SIMBA YACHAPWA , HARUSI YAGEUKA MSIBA TAIFA


Simba wakiwapungia mikono mashabiki kabla ya mechi


SIMBA SC imefungwa mabao 3-1 na Nairobi City Stars katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii katika mechi iliyochezwa sambamba na Simba Day.
Lakini kufungwa huko kwa Simba kulitokana na kocha Milovan Cirkovick kubadilisha karibu kikosi kizima kilichoanza na kuingiza wachezaji wapya, ambao waliitoa City Stars ya Nairobi nyuma kwa 1-0 na kuipa ushindi wa 3-1.
Simba ilitangulia kupata bao kupitia kwa Felix Sunzu dakika ya 15, pasi ya Mwinyi Kazimot na ilikwenda kupiumzika ikiwa mbele kwa bao hilo.
Lakini kipindi cha pili, kipa aliyempokea Juma Kaseja, Hamadi Waziri alitunguliwa mabao matatu katika dakika 57 na Duncan Owiti, dakika ya 64 na Bruno Okullu na dakika ya 79 na Boniphace Onyango.  
Mapema katika tamasha hilo, Simba ilitoa tuzo mbalimbali kwa wachezaji wa sasa na wa zamani kwa mchango wao kwenye klabu hiyo, pamoja na baadhi ya wadau wake.
Waliopewa tuzo kwa wachezaji wa sasa, ni Shomary Kapombe (Nidhamu), Emmanuel Okwi (Mchezaji bora wa msimu) na marehemu Patrick Mfisango (Heshima).
Wa zamani ni Haidari Abeid ‘Muchacho’ (Mchezaji Bora miaka ya 1970), Hamisi Kilomoni (Mchezaji Bora Miaka ya 1960), Ally Sykes (Heshima, Udhamini), Profesa Philemon Sarungi (Mchango wa muda mrefu klabuni) na Gaorge Kavishe, Meneja wa Kilimanjaro Beer, Wadhamini wa sasa wa Simba SC.
Katika mechi ya kwanza, timu na wanawake ya Simba, Simba Queens mchana wa leo, iliifunga Ever Green ya Temeke mabao 5-3 katika mchezo wa Ligi ya Wanawake, Dar es Salaam uliokwenda sambamba na tamasha la Simba Day, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ngassa anasikitika baada ya kukosa bao la wazi

Boban kazini

Uhuru anakwatuliwa

KIKOSI CHA SIMBA
1. JUMA KASEJA
2. CHOLO NASSOR SAID
3. AMIR MAFTAH
4. JUMA NYOSSO
5. SHAMTE HARUNA
6. MWINYI KAZIMOTO
7. SILIM KINJE
8. HARUNA MOSHI(BOBAN)
9. MRISHO NGASSA
10. FELIX SUNZU
11. UHURU SULEIMAN
                       


0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine