Tuesday, August 14, 2012

Wenger : Asernal iko imara inaweza kutwaa mataji.


Arsene Wenger anaamini kuwa Arsenal inaweza kupigania mataji msimu baada ya kuwa katika kipindi kizuri cha kuwa wachezaji wake muhimu ambao walikuwa majeruhi huko nyuma.
Mfaransa huyo tayari ana uhakika wa kupata huduma za wachezaji Lukas Podolski, Olivier Giroud na Santi Carzola, na kizuri zaidi ni Robin van Persie kusalia katika klabu hiyo licha ya taarifa za kutaka kuondoka kushika kasi.
Wenge mwenye umri wa miaka 62 anashukuru maandalizi ya kuanza msimu kwenda vizuri lakini pia katika hicho chote kikosi chake kuepuka kupata majehihi.
Anasema kwasasa kikosi kiko tayari kukabiliana na chanagamoto za kuwania mataji ukilinganisha na msimu uliopita.
amenukuliwa akisema
"tuko katika hali imara kuliko msimu uliopita ambapo tuliwapoteza Nasri na Fabregas ambao waliondoka lakini zaidi ya hapo tuliwapoteza pia Diaby na Wilshere ambao walikuwa majeruhi" .
"hivyo tulipoteza wachezaji wanne wakati wa kuanza msimu tofauti na wakati huu,tunataka kushindana na hiyo ndiyo nia yetu.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine