UTANGULIZI
Mpendwa mtumiaji wa site hii ya pekee katika maisha ya afya yako,
yote yaliyoandikwa humu si porojo. Kutumia mimea ya asili katika kutibu maradhi
(magonjwa ) ni suala la muhimu sana
katika wakati huu tulio nao.
Kwani dawa za viwandani zina bei ya juu sana na upatikanaji wake huwa ni mgumu pia
aina nyingi za madawa hayo zina madhara baadae kwa binadamu hasa
ukiyatumia kwa muda mrefu.
Utumiaji wa mimea katika suala umethibitishwa na wataalamu wengi duniani
siku hizi. Kutumia maua , majani, magome ya miti
na mizizi na matunda, katika suala la kutibu maradhi siyo ushenzi au upagani kama wengine wanavyodhani kwani hata dawa za viwandani ni
matokeo ya mimea isipokuwa zile za ki-biologia na kikemikali.
Mimea kama kitunguu swaumu, mdalasini, kitunguu maji, avokaldo,
tangawizi, papai, aloe vera, matango n.k hutibu magonjwa mengi yanayomkabili
binadamu kama vile: kansa, kisukari, kuhara,
kupooza, n:k
Maji pia ni kiburudisho na ni dawa tangu zama za kale. Biblia
imethibitisha ukweli huo kwani zama za manabii, jemedari mmoja mkoma
aliambiwa ajitose majini kwa utaratibu kama
alivyoambiwa, akafanya hivyo…akapona. Hata zamani za yesu kristo maji
yalitumika sana kama
dawa. kwani hata chakula tulacho pasipo maji hakiwezi kumeng’enywa na
vimeng’enya. Vimeng’enya husaidiwa na maji, kwa hiyo maji na dawa nje na ndani
ya mwili. Hivyo basi bila maji hakuna uhai.
VITUNGUU SWAUMU
Kitunguu swaumu chaweza kutibu magonjwa mengi ikiwa mgonjwa atafuata
maelekezo vizuri . katakata kitunguu swaumu saizi ya vidonge kasha umeze kwa
kutumia maziwa ya moto.
KITUNGUU SWAUMU HUTIBU
MAGONJWA YAFUATAYO
BRONHITIS (MKAMBA):
Ugonjwa wa kifua au mkamba ni mwambukizo wa mifereji inayoingiza hewa
mapafuni, hii husababisha kikohozi chenye sauti mara kwa mara ikiambatana na
kutoa makohozi mazito.
DIARHOHEA (KUHARA):
Ugonjwa wa hatari wa kuharisha dalili zake ni kupata choo chenye maji
maji zaidi ya mara 6 katika masaa 12
HARDENNING OF HARTERIES:
Tatizo katika mishipa ya damu inayochukua hewa safi , mishipa hiyo ambayo huwa miepesi na
laini huwa migumu na kushindwa kufanya kazi yake na kuhatarisha maisha ya
muhusika.
INTESTINAL PARASITE
Hawa ni wadudu wadogo wadogo ambao hujificha ndani ya utumbo mdogo tene
ni wakubwa kuliko backteria.
HAEMORRHOIDS/ PILE (RUTUNI):
Nimishipa ya damu inayovimba na kukunjamana na kujitokeza katika njia ya
haja kubwa, husababisha maumivu makali wengine huuita kutoka mgongo.
VARICOSIS / VARICOSE VEIN
(MISHIPA YA DAMU ILIYOVIMBA)
Hii ni mishipa ya damu iliyovimba, hukunjana na kuuma sana . Mara nyingi huonakana katika miguu ya
watu wa makamo na akina mama wajawazito na waliuokwasha zaa watoto wengi.
KIDNEY DISEASES (MAGONJWA YA
FIGO):
Kuna matatizo mengi ya figo na njia ya mkojo, mara nyingi si rahisi
kuyatofautisha. Dalii :- Maumivu katikati ya mgongo au kiuno, ambayo
yanaenea mpaka sehemu ya juu ya tumbo na chini ya mbavu, Dalili nyingine
ni damu kwenye mkojo na uvimbe utosini.
OBESITY (UNENE)
Ni unene unaopita kipimo, mara nyingi husababisha matatizo mengi kama vili ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa figo na mshuko
(stroke). Watu wanene ndio hasa wanaweza kuwa na blood pressure
PIMPLES (CHUNUSI)
Ni viuvimbe vidogo vidogo vilivyo na ncha nyeupe ya usaha, au ncha
nyeupe ya uchafu. Mara nyingi vinaweza kuuma au kutanuka.
HYSTERIA:
Ugonjwa wa kuweweseka upweke, husababisha chembe Fulani ya ubongo
kutodaka mambo kadhaa ya lazima kwake . ugonjwa huu huwapata wanawake na hasa
wasichana katika shule zisizo za mchanganyiko.
SKIN DISEASES
Ni magonjwa mbalimbali ya ngozi kama
vile:
-IMPERTIGO CONTAGIOSA (mzio wa ngozi)
-BAKAMBA SHINGLES / HERPES ZOSTER
CUSTO / FEAR (WOGA)
Mtu mwenye custo huwa na woga wasi wasi mwingi na ni mwoga, na mtu huyu
anaweza kuanza kutetemeka, tabia isiyo ya kawaida, kukondeana na mwisho kufa.
RHEUMATIC (UGONJWA WA
KUKAKAMAA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI):
Kuna aina 3 za ugonjwa huu:-
1.Rheumatic ya mifupa
2. Rheumatic ya misuli
3. Rheumatic ya viungo
MUSCLES INFLAMATION:
Shida katika misuli.
CONSTIPATION (KUFUNGA CHOO):
Mtu ambaye hapati choo kwa muda wa siku 2 au zaidi. Anshauliwa kutumia
kitunguu swaumu.
TYPHOID FEVER (HOMA YA
MATUMBO)
Hii ni homa inayoambukiza utumbo na kusababisha maumivu makali mwili
mzima. Dalili zake ni sawa na zile za malaria.
MATATIZO YA INI
Mtu hukosa kabisa hamu ya kula, hapendi kula, hutaka kutapika, macho na
ngozi hubadilika rangi na kuwa ya njano, choo huwa cheupe.
HOARSE VOICE / LARYNGITIS:
Sauti kutotoka sawa sawa, au kutoa sauti ya mikwaruzo.
Kutokana au ugonjwa wa kifuko cha sauti
NEUROSIS
Shida katika mishipa ya fahamu
METABOLIC DISORDERS:
Kushindwa kuyeyusha chakula
GALLSTONE (UCHAFU ULIO NDANI
YA KIFUKO CHA NYONGO)
Mara nyingi nyongo husaidia kuyeyusha vyakula vya mafuta , uchafu ulio
ndani ya nyongo husababisha nyongo isifanye kazi vizuri , na wakati mwingine
nyongo hudhurika.
EYE SIGHT DISEASES
uwezo wa kuona sawasawa.
ANOREXIA / LOSS OF APPETITE:
Kukosa hamu ya kula
COUGHS
Kukohoa au kikohozi
ASTHMA
Shida ya pumu, kubanwa katika mapafu na kushindwa kupumua ghafla..
UTAYARISHJI WA KITUNGUU SWAUMU
SWAUMU KWA AJILI YA MATIBABU YA MARALIA
Chukua punje 6 mpaka 7 za vitunguu swaumu, menya kisha vikatekate saizi
ya vidonge, vimeze kwa maziwa ya moto au maji/ mara 3 kwa siku kwa muda wa siku
14. kwa magonjwa mengine yaliyoandikwa humu vimeze kwa muda mrefu maana hutibu kama chakula.
0 comments:
Post a Comment