Sidhani kama kuna asiyependa kuwa milionea.wengi wetu tumekuwa na ndoto ya
kufanikisha malengo yetu.Kuna kitu kimoja cha kujiuliza hapo!
Tunawezaje kufika hapo? Majibu yake ni mepesi kuliko unavyoweza
kuichosha akili yako kwa mawazo.Hizi ni baadhi ya njia tano kuu za
kukufikisha kwenye uwanja wa mamilionea!!!
Hizi ni baadhi ya njia tano kuu za kukufikisha kwenye uwanja wa mamilionea!!!
1.Oa mara moja tu.
Njia hii inamwezesha mtu kuwa milionea kwa kuwa na familia ya watoto wasiozidi watatu,na mke mwenye kuipangilia familia bajeti ya kawaida!
2.Usiishi kwa kutegemea kipato kimoja tu.
Kuoa
ama kuolewa, ni kuunganisha pia nguvu kazi kati ya wawili hao. Hata
kama mmoja ana kazi na mwingine hana, mnaweza kuunganisha maarifa ya
nini cha kufanya ili kuwe na mfumo mwingine wa kipato cha ziada.
3.Kuwa tayari kujifunza.
Hakikisha kila siku unajifunza kitu kipya kutoka watu waliokuzunguka na kukuzidi au wapo juu yako kifikra au kipato chao kimekuzidi wewe.Usiache hata siku moja siku ipite bila kusoma kitabu au kupata mafunzo mapya yanayohusiana na maisha yako na shughuli uifanyayo.
4.Wekeza fedha zako katika samani.
Tunashauriwa
kuwekeza katika vitu vyenye thamani kuliko kuzitumia pesa bila
mpangilio.Maisha yanabadilika, na huwezi jua ni lini mkondo wako
utayumba na kuhitaji njia mbadala ya kukurejesha katika hali ya nyuma
uliyokuwa nayo.Kwa kununua mali zenye thamani, itakusaidia kwa kuviuza
pale mambo yanapokwama, na kuzitumia kuzalisha vingine na vingine zaidi.
5.Usiishi maisha ya kimilionea.
Unaweza
kuishi maisha ya kawaida na kwa muonekano wa kawaida katika macho ya
watu,kutakakokusaidia ku-maintain kipato chako vizuri kimatumizi.Kama
tunavyojua,ukiishi maisha ya juu,ndivyo mahitaji nayo yanakuwa ya hali
ya juu.
0 comments:
Post a Comment