Thursday, July 14, 2011

ROSTAM AZIZ AJIVUA GAMBA RASMI..


Mbunge wa Igunga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, ambaye pia ni mfanyabiashara mkubwa nchini Tanzania, Rostam Aziz, ameachia ngazi hiyo jana! Akiongea na wapiga kura wake jimboni kwake Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora, Rostam alitamka kuwa ameamua kuachana na SIASA UCHWARA ili apate muda wa kufanya biashara zake. 
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wanahabari, alitangaza kuachia ngaza nafasi yake ya ubunge wa Igunga na ile ya ujumbe wa NEC! Hii ina maana kwamba Rostam ameamua kujivua gamba mwenyewe kabla ya kuvuliwa na kwamba jimbo la Igunga sasa liko wazi.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine