Thursday, July 14, 2011

SAFARI YA MWISHO YA MENEJA WA FM ACADEMIA.

MAZISHI ya aliyekuwa meneja wa bendi ya Fm Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Boniface Kasanju  ‘Bonny Manjonjo’,  yaliyofanyika jana katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam,  yaligubikwa na vilio na majonzi kwa waombolezaji waliohudhuria.
Ibada ya kuaga mwili wa marehemu ilifanyika  katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Magomeni ambapo ilihudhuriwa na watu  mbalimbali wakiwemo wanamuziki, wanamichezo, mashabiki, ndugu jamaa na marafiki. 


Mwili wa marehemu Boniface Kasanju ukiwa kanisani wakati wa kuagwa


Watoto wakiaga mwili wa baba yao. 

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine