Wednesday, July 13, 2011

STEPHEN MWASIKA NJE YA UWANJA MIEZI MITATU.

BEKI wa pembeni wa Yanga, Stephen Mwasika anatarajiwa kurejea uwanjani baada ya miezi mitatu kufuatia kufanyiwa operesheni ya goti.

Beki huyo alirejea nchini hivi karibuni akitokea India alipokwenda kufanyiwa upasuaji huo baada ya kupata majeraha kwenye mechi za mwisho za Ligi Kuu ya Vodacom.

 “Ndugu kwanza kabisa nashukuru kwa kufanyiwa operesheni, kila siku nilikuwa nafikiria hatma yangu hali iliyokuwa ikinifanya nikate tamaa ya kucheza tena soka.

“Mashabiki wa Yanga wanatakiwa kuniombea ili afya yangu ikae vizuri na hatimaye nirejee uwanjani mapema,” alisema Mwasika na kuongeza:

“Kwa mujibu wa madaktari wangu, nitarejea uwanjani baada ya miezi mitatu lakini kwa kuanza na mazoezi binafsi huku nikipata huduma ndogo ndogo kwenye Hospitali ya Agakhan ya jijini Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine