Monday, August 22, 2011

STAA wa tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ (pichani) amejigamba kuwa mambo yake ni mazito kuanzia suala zima la mapenzi na kujikamilisha kimaisha huku akitangaza dau kwa mwanaume anayetaka kumuoa bila kujali kuwa umri wake mdogo wa miaka 18.

Akizungumza na The Biggest IQ Paper Bongo, Ijumaa Wikienda, jijini Dar juzi, Lulu aliweka kweupe kuwa yeye ni mwanamke aliyejikamilisha kila idara.

“Sipendi kusema kwa maneno ila mwanaume atakayenioa atajionea mwenyewe kwani nimejikamilisha kuanzia mambo ya chumbani hadi mpango mzima wa kuyamudu maisha,” alisema Lulu na kuongeza:
“Kuhusu mahari yangu, unajua mimi ni mchaga kwa hiyo itategemea, lakini hata kama ni shilingi laki tano poa tu kwani ‘kinachomata’ ni mapenzi ya dhati na siyo dau kubwa la mahari.”

Wakati huo huo, kesi iliyokuwa ikimkabili Lulu akidaiwa kumtukana Kilakhaba Aziz, mkazi wa Dar katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni chini ya Hakimu Marko Mochiwa, Agosti 18, mwaka huu, ilifutwa kutokana na mlalamikaji kutofika mahakamani kila ilipotakiwa kusikilizwa.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine