Monday, August 22, 2011

MSONDO WANJAKWA TUZO NAIROBI, KENYA

BENDI ya muziki ya Msondo Ngoma Band ya Tanzania imetwaa tuzo ya The Best Rhumba Group katika East Africa Music Awards, mashindano yaliyofanyika mjini Nairobi Kenya, yaliyoshirikisha bendi za Afrika Mashariki na Kati ambapo  iliibuka kidedea mwishoni mwa wiki.

Hayo yalithibitishwa na msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila  au Super D aliyesema kwamba watahakikisha wanawaonyesha mashabiki wao kilichowafanya kupata tuzo hiyo.

Super D alisema itanza mazoezi leo (Jumatatu) kwa ajili ya kujiandaa na
sikukuu ya Iddi inayotarajiwa wiki ijayo ambapo wanaingia kambini kusuka vibao vipya na kuvifanyia kazi.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine