Sunday, November 20, 2011

HAYA NDIO MAPATO YA TANZANIA NA CHAD.

Pambano la mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil- raundi ya mtoano kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Chad lililochezwa Novemba 15 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 78,389,000. Mashabiki waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo ni 29,111. Viti vya kijani na bluu ambavyo kiingilio kilikuwa sh. 2,000 ndivyo vilivyovutia mashabiki wengi ambapo walikuwa 23,748 ikiwa ni zaidi ya asilimia 80 ya mashabiki wote walinunua tiketi kwa ajili ya viti hivyo. VIP A ambapo ndipo kulikokuwa na kiingilio cha juu cha sh. 20,000, jumla ya mashabiki 187 walinunua tiketi kwa ajili ya eneo hilo. VIP B ambapo kiingilio kilikuwa sh. 10,000, mashabiki walionunua tiketi walikuwa 1,181. Viingilio vingine katika pambano hilo vilikuwa sh. 5,000 kwa VIP C ambapo waliingia mashabiki 1,678 wakati mashabiki 2,319 walikata tiketi kwa viti vya rangi ya chungwa ambapo kiingilio kilikuwa sh. 3,000.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine