MOVIES star wa Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, maisha yake ya sasa hayaeleweki, anadaiwa kuwa hana pa kuishi na amekuwa akiweka kambi popote giza linapomkuta, The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda lina fulu data.
Uchunguzi wa gazeti hili kupitia mashosti wa karibu wa msanii huyo umebaini kuwa kwa sasa maisha ya Kabula ambaye mara ya mwisho alikuwa akiishi kwa bosi wake, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ maeneo ya Makongo Juu, Dar es Salaam ni ya kutapatapa kwani amekuwa ‘akiangusha gari’ popote giza linapomkuta.
“Ukimpigia simu asubuhi hii, utagundua kabisa hana sehemu maalum ya kulala kwa sababu nimemuacha amelala Mwananyamala kwa Rehema (Fabian) na jana tu alilala kwa shosti wake maeneo ya Kinondoni. Hapo alipo sasa ana safari tena ya kwenda Tabata kwa rafiki yake anayeishi naye, kwa jumla maisha yake si mazuri na kiukweli kabisa anahitaji ushauri,” alisema rafiki wa karibu wa staa huyo.
Baada ya kusikia ishu hiyo, ‘polisi’ wetu alisaga lami hadi nyumbani kwa Mshiriki wa Miss Kiswahili 2009, Rehema Fabian ambapo alimkuta Kabula akiwa ‘amembonji’ jambo ambalo lilithibitishia maelezo ya ‘sosi’.
Ilibidi kumhoji Rehema juu ya maisha ya mwenzake kama kweli hana makazi maalum ambapo alifunguka:
“Mara nyingi Kabula huwa akilewa sana au akichelewa kurudi Tabata analala kwangu, mimi naona imekuwa kawaida yake ‘so’ sioni kama kuna tatizo kwa sababu ni rafiki yangu wa kitambo.
0 comments:
Post a Comment