Wakali wa tasnia ya muziki wa hapa nyumbani Tanzania Mwana FA kutoka upande wa bongoflava na mwenzake Khalidi Chokoraa anayefanya muziki wa dansi wameamua kuonesha umwamba wao kwenye swala zima la kurusha makonde.Uamuzi huo umekuja baada ya wasanii hao wawili kukubaliana kuwa watapambana live kwenye pambano litakalofanyika desemba 18 pale kwenye ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo Millenium Tower kijitonyama,ambapo siku hiyo mbabe kati yao atajulikana,ambapo pambano hilo litakuwa la raundi 3,pambano hilo litakuwa la utangulizi kwenye kuwania ubingwa wa Afrika kati ya Ibrahim Nuksi wa Rwanda na Mrisho Rajab wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment