Thursday, March 29, 2012

ALICHOSEMA ONE BAADA YA KUPOKEA MSG YA NIKKI WA PILI.

.
Rapper One ambae anafanya kazi na M-Lab studios, amekubali kutoa ufafanuzi wa status yake ya jana kwenye mtandao wa facebook ambayo ilimuhusu rapper kutoka kundi la Weusi, Nikki wa pili.
One amesema “chanzo cha kuandia hiyo status ni kwa sababu Nikki wa pili amemtumia msg Nikki Mbishi msg ambayo Mbishi alinifowadia, ilikua inasema kwamba sisi bado ni wadogo kwenye muziki na hatuwezi rap, pia album ya Mbishi inasound kama single moja…. sasa mimi sikuona sababu ya yeye kunihusisha mimi kwa sababu sijawahi kumzungumzia Nikki na wala sikumbuki kama kuna siku nilishaongea nae chochote hata siku moja”
Ameamplfy zaidi kwamba “kuna track moja nilishafanya pale Tongwe ambayo kuna mstari nilisema siwezi kuuza kura yangu kama Bonta, sasa nashangaa sasa hivi niko kwenye beef na weusi wakati sielewe chochote, juzi juzi tu nimezungumza na Lord Eyes na Joh Makini na hakukua na dalili zozote za kuwepo beef manake tuliongea vizuri tu hata kesho yake Joh alinipigia simu akaniuliza kama nilifika salama na nilipenda sana kwa sababu yeye ni kama kaka, ofcourse mi nilitegemea response ingetoka kwa Bonta na sio wengine kwa sababu sikuwaongelea kwenye hiyo track”
Kwa kumalizia One amesema “baada ya kupata hiyo msg nilishindwa kumchek Nikki wa Pili kwa sababu kwanza sina namba yake na pia nilishapata uthibitisho toka mwanzo kwamba alikataa kufanya track na STEREO kwa kisingizi cha kwamba mimi nimemdiss Bonta na Nikki, all this time nimekaa kimya huyu mtu hapati picha kwamba mimi sina habari na yeye? naona amevuka mipaka, haelewi kwamba mimi sina habari na yeye,  mimi sina beef na wala sina huo muda kwahiyo kama sijakuongelea basi usinihusishe kwenye maongezi yako”

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine