Thursday, March 29, 2012

KESI YA SERUKAMBA YAFUTWA.

Peter Serukamba.
Jaji wa mahakama kuu kanda ya Tabora Stella Mugasha amefuta kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Ubunge, iliyokua inamkabili mbunge wa jimbo la kigoma mjini Peter Serukamba, kutokana na upande wa madai kukaidi amri ya mahakama kwa kushindwa kupelea mashahidi.
Mwanzoni mawakili wa upande wa mdai ambae ni Ally Mleh  walijitoa katika kesi hiyo kwa kile walichodai kutoridhishwa na mwenendo wa kesi, na hivyo mlalamikaji kuomba apewe muda wa kutafuta mawakili wengine lakini alishindwa huku akipinga kesi hiyo kuendelea kusikilizwa na jaji Mugasha.
.
Baada ya uamuzi huo kutangazwa, Serukamba amesema “nimefurahi sana kwa sababu haki imetendeka na imeonyesha mahakamani sio sehemu ya kupelekwa majungu, sio sehemu ya kupeleka maneno ya kwenye vijiwe vya kahawa kwa sababu ukiangalia kesi yenyewe ni kesi tu ya watu ilitengenezwa kutokana na kujaa chuki, lakini wao wenyewe wamekuja kushindwa kuiendesha kesi yao na mawakili wao wamejitoa”
Ally Mleh ambae ndo mdai, amesema “uamuzi uliotolewa na mahakama unamkatisha tamaa yeye na watanzania kwa sababu tulipokwenda mahakamani mwanzoni tulikua tunaamini kwamba Mahakama itatenda haki ya mdai na wadaiwa, kwa sasa hivi sina imani kabisa na kutokana na uamuzi uliotolewa na jaji huyu, kwa hiyo nitakata rufaa katika mahakama kuu ya rufaa na ina maana haki yangu itatendeka”

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine