Monday, March 5, 2012

Chelsea yamfukuza Kocha Villas Boas


Habari moto moto kutoka mtandao wa klabu ya Chelsea inayocheza katika Ligi kuu ya England, zasema kua klabu hio imeachana na kocha Andre Villas-Boas leo jumapili.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 34 amepoteza kazi hio saa 24 baada ya kupoteza jana pambano la Ligi dhidi ya klabu ya West Bromwich Albion 1-0.

Kufuatia mechi ya jana Chelsea ilijikuta katika nafasi ya tano kweenye msimamo wa Ligi.
Tangazo la Chelsea limesema kua aliyekua naibu wa Kocha huyo Roberto Di Matteo atashikilia wadhifa wa Kocha hadi mwisho wa msimu.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine