Mkali wa Soka , Nyota -a.k.a- (Super Star) wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amesababisha mshtuko, kelele pamoja na ghasia takatifu wakati alipopaki gari lake jipya (Super Car) katika moja ya mitaa ya Lisbon. Gari hilo linakwenda kwa jina la 'Batmobile' Ferrari.
Kijana huyu aliyekuwa mchezaji machachari na adui wa nyavu za wapinzani wa Manchester United ambaye pia ni mchezaji wa kimataifa wa Ureno, alipigwa picha pindi alipokuwa akijipatia chakula ya jioni katika moja ya migahawa ya Kijapani inayopatikana katika jiji la Lisbon-nchini Ureno.Hata hivyo,ni gari lake tu lililopewa umuhimu mkubwa kwa kushangaliwa ambapo lilionekana kuwa kitendawili kwa Wareno waliokumbana nalo kwenye Parking.
Tovuti moja ya michezo ya Ureno(globoesporte.com) imetangaza kwamba, picha hiyo hapo juu inaonyesha kwamba Ronaldo huenda amechukua baadhi ya miongozo (au wahyi ) kutoka -Dark Night- wakati wa kuchagua safari yake.
Gari hili ambalo limepewa jina la utani -'Batmobile'-kutokana na sababu zilizo wazi kabisa na zinazoweza kuonekana kwa macho, litaleta matumaini makubwa katika miliki au mali za Cristiano Ronaldo kuliko lile gari jekundu Ferrari 599 alilokuwa akiliendesha alipokuwa Manchester United.
Gari hilo lilipoteza umaarufu wake mapema kabla ya wakati wake baada ya kupata ajali ya kuanguka likiwa kwenye zile barabara za chini kwa chini (chini ya hadaki) kwenye A538 karibu na uwanja wa ndege wa Manchester.
Gari hilo liliharibika na kuwa nyan'ga nya'nga,lakini kwa bahati nzuri Ronaldo alibahatika kutoka salama ndani ya gari hilo pasina kupata jeraha lolote. Huenda kwa ajili ya usalama wake zaidi, ikawa ndio sababu iliyopelekea au liyochochea mkali huyu Cristiano
Ronaldo kuwekeza katika gari jingine la ukweli. Alipokuwa Manchester United alikimiliki gari nyekundu ambayo ilioneka na kuwa na mikosi, maana haikuchelewa kupoteza umaarafu wake pindi ilipopata ajali.
Lakini Mara hii ameamua kufanya mabadiliko kidogo na kuingia na 'Kitu Black' , ukiichunguza vizuri gari hii utagundua kuwa kila sehemu ni nyeusi,ikiwemo na tairi zake.
Viti viwili vya 599 GBT Fiorano vinavyopatikana ndani ya gari hili,gharama yake pale maeneo ya Uingereza ni:
Euro £212,000 , gari hii pia lina Injini inayotumia lita 6.0 - v12 , na 612bhp. Linaweza kutumia 62mph kwa sekunde 3.7 tu, na kwenda hadi kwenye 205mph.
0 comments:
Post a Comment