John Boko wa pili kutoka kulia.
Baada ya kuendelea kuzomewa mfululizo na mashabiki wa soka wakati akiwa anaichezea timu ya taifa, John Bocco ameamua kustaafu kuitumikia timu ya taifa ili kuepukana na shida anazozipata kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo ya taifa.
Bocco ndio amekuwa mchezaji anayezomewa sana wakati anapoichezea timu ya taifa, jambo ambalo limekuwa likimkosesha raha na amani kwa muda mrefu anapokuwa akiitumikia timu ya taifa lake.
“Nimefikia maamuzi haya baada ya kufikiria sana, nimekuwa nikijitoa kwa hali na mali kulitumikia taifa langu lakini mashabiki wa timu yetu wanaona sifai, hivyo ni bora nijitoe au nistaafu kuichezea timu hiyo ili kuepukana na hilo. Naitakia kila kheri timu yangu ya taifa naipenda na nitaendelea kuipenda siku zote.” – John Bocco
Habari kutoka kwa shaffihdauda.com
0 comments:
Post a Comment