Monday, April 30, 2012

AUNT, ISHA KWENYE BIFU ZITOOO...





Na Imelda Mtema
MWIGIZAJI wa filamu za Kibongo,  Aunt Ezekiel na mwimbaji wa Taarab, Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’ wamezua timbwili kisa kikidaiwa kuwa ni mwanaume, Ijumaa Wikienda lina kila kitu.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lilitokea Ijumaa, saa 10 alfajiri katika pub inayomilikiwa na Aunty iliyopo Mwananyamala Gereji, jijini Dar baada ya Mashauzi kufika akiwa na wenzake sambamba na mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Jumanne.
“Walipofika walitaka kuhudumiwa, Aunt akakataa kwa madai kuwa tayari alishafunga,” kilisema chanzo chetu na kuongeza kuwa visa kati ya wawili hao vilianza siku kadhaa zilizopita baada ya Isha kumtuhumu Aunt kuwa anatoka na Jumanne.
Baada ya kunyimwa huduma, Isha alianza kurusha vijembe kwa Aunt, naye akajibu mapigo kwa kuanza kumponda Jumanne kuwa aache kujisifu kuwa anatoka naye kimapenzi.
Katika timbwili hilo, Aunt alimsukuma Jumanne aliyeangukia kwenye viti, hali iliyomfedhehesha sana, akampiga marufuku ya kufika kwenye pub yake.
Jitihada za kuwapata wahusika kuzungumzia sakata hilo hazikuweza kufanikiwa.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine