Habari zinasema kuwa katika suala la usafiri tu amekuwa akitumia gari la kifahari la kukodi, Range Rover, anayolipia Sh 450,000 kwa siku. Mwanadada huyu ambaye mara nyingi filamu zake ni moja kati ya filamu ambazo hufanya vizuri sokoni, anaishi Kijitonyama katika moja ya nyumba yenye aliyopanga baada ya kuondoka kwao Mbezi. Inasemekana kuwa Irene hapendi kutumia aina ya gari ambayo hata wasanii wengine wanaweza kutumia. Lakini sasa imeelezwa ameachana na Range hiyo na amekodi Hammer ambayo kila baada ya siku nne anailipia Sh 4 milioni. Mwanaspoti iliongea na mmiliki wa magari hayo na kuthibitisha kulipwa fedha hizo na Uwoya. Hata hivyo mmiliki huyo hakupenda kutajwa jina gazetini. |
1 comments:
oya mbona habari inaishia njian
Post a Comment