Rashidi Yekini enzi za uhai wake.
Rashidi Yekini alizaliwa katika jimbo la Kaduna mwaka 1963. Baada ya
kuanza kucheza kandanda ya kulipwa kwenye ligi nchini Nigeria, alikwenda
Ivory Coast kuichezea klabu ya Africa Sports. Baada ya hapo alitimkia
Ureno ambako alikuwa mfungaji mabao hodari katika ligi ya daraja la
kwanza ya Ureno ambapo msimu wa 1993–94 alikuwa amepachika mabao 34
katika mechi 32 alizocheza.
Kupanda kwa kiwango chake cha usakataji kabumbu akiichezea timu ya
taifa ya Nigeria msimu huo ambapo Nigeria ilishiriki kwa mara ya kwanza
mashindano ya Kombe la Dunia na baadae kufuatiwa na Kombe la Mataifa ya
Afrika, alitunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika mwaka 1993, akiwa
mchezaji wa kwanza wa Nigeria kupata tuzo hiyo.
Rashid Yekini, ambaye alikuwa ametalikiana na mkewe tangu mwaka 1994
alikuwa akiishi maisha ya tabu na wapangaji wengine wachahe katika
nyumba yake mjini Ibadan, jimbo la Oyo ambapo iliarifiwa mara chache
sana alikuwa akitembelewa na wageni.
Yekini amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 49. Ameacha watoto
wawili. Anazikwa kesho Jumapili kwa mujibu wa taratibu za dini ya
Kiislamu huko Irah, jimbo la Kwara.
0 comments:
Post a Comment