Wastara
ambae ni Mke wa mwigizaji wa movie za kitanzania SAJUKI akiwa mgonjwa
sasa hivi, amethibitisha kwamba pesa zisizopungua laki nane za
kitanzania nimeibiwa kwenye account yake ya simu ya mkononi aliyokua
anaitumia kupokelea pesa za msaada wa watanzania kumsaidia Sajuki kwenda
kutibiwa.
Wastara
ameiambia millardayo.com kwamba “ni kweli msg zilikua ni nyingi sana na
kabla ya kuingia kwenye kipindi cha Leo tena CLOUDS FM kilichoendesha
zoezi la kuchangia, simu ilikua ina pesa kidogo lakini cha ajabu nikaja
kukuta hela ni ndogo kuliko msg zilizokuwepo pia baada ya hapo msg
zikagoma kuendelea kuingia”
“kwa
haraka haraka pesa iliyochukuliwa ni zaidi ya laki nane, na
tulichokifanya tumemuomba mkurugenzi aiblock hiyo namba ili tuone kama
zimeshatolewa au bado na ninategemea kwenda kwenye ofisi zao wakala
manake hii sio mara ya kwanza kuibiwa, nilishawahi kuitangaza namba
kupitia CLOUDS FM siku moja lakini siku ya pili tu zikaibiwa pesa zote
ambazo ni laki nne, nilifatilia lakini mwisho wa siku akaja kulipa
wakala wenyewe wenye shirika wakasema hawahusiki”
Mpaka
sasa bado Wastara anaendelea kumtafuta mtu alieweza ku-hack simu yake
na kuzimiliki hizo pesa ambazo anatumiwa kwa njia ya simu ya mkononi,
millardayo.com inaendelea kufatilia…. kama kutakua na chochote cha ziada
utafahamu kupitia hapahapa.
story from: www.millardayo.com
0 comments:
Post a Comment