skip to main |
skip to sidebar
5/10/2012 07:44:00 AM
Unknown
No comments
TIMU ya soka ya Simba imeondoka jana jijini Dar es Salaam kwenda Sudan
kwa ajili ya mechi ya marudiano ya michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF)
dhidi ya timu ya Al Ahly Shandi ya Sudan.
Msafara wa Simba utakuwa na wachezaji 19 na viongozi saba.
Wachezaji wanaoondoka ni Juma Kaseja, Ally Mustafa, Shomari Kapombe,
Derick Walulya, Amir Maftah, Juma Jabu, Obadia Mungusa, Kelvin Yondani,
Victor Costa, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Patrick Mafisango, Haruna
Moshi, Machaku Salum na Uhuru Selemani.
Wengine ni Felix Mumba Sunzu, Emmanuel Arnold Okwi, Edward Christopher
Shija na Gervais Arnold Kago.
Viongozi wanaofuatana na timu hiyo ni Ismail Aden Rage (MB), Swedy
Fikirini Mkwabi, Milovan Cirkovic, Amatre Richard, James Stephan Kisaka,
Dk. Cosmas Kapinga, Nicholaus Menrad Nyagawa na Ezekiel Kamwaga.
Mkuu wa msafara huo atakuwa ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Hussein Mwamba.
Wachezaji wawili; Nassor Said Masoud (Chollo) na Juma Said Nyoso
hawatakwenda Sudan kwa vile wanatumikia adhabu zao za kukosa mechi
kutokana na kuwa na kadi.
Mechi ya Shandi na Simba itapigwa Jumapili ijayo katika Uwanja wa Shandi
wenye uwezo wa kuchukua washabiki 10,000.
Mji wa Shandi uko Kaskazini Magharibi mwa Sudan na uko umbali wa
kilomita 150 kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.
0 comments:
Post a Comment