Msanii
wa filamu Juma Kilowoko maarufu kwa jina la Sajuki ambaye anasumbuliwa
na maradhi ya uvimbe tumboni kwa muda mrefu sasa anaondoka nchini leo
kuelekea India kwa matibabu yake baada ya kusumbuliwa na ugonjwa huo na
kukosa matibabu hapa nchini. Safari ya msanii huyo imekuja baada ya
wadau wa filamu, wasanii na
watu mbalimbali
kujitolea kwa nyakayi tofauti ili kuweza kufanikisha matibabu ya msanii
huyo wa siku nyingi ambaye pia ni Director, Jumla ya Tsh. 16 milioni
ziliweza kupatikana huku ikiwa bado inahitajika Tsh. 9 milioni ili
kukamilisha kiwango kilichokusudiwa kukusanywa kwa ajili ya matibabu ya
msanii huyo, na pia ziliweza kupatikana tiketi tatu za ndege za kwenda
na kurudi nchini India.Tunakutakia kila la kheri Sajuki na Mungu
akubaliki.
0 comments:
Post a Comment