Utaratibu
wa timu za kisudani kuzipokea vibaya timu pinzani zinapoenda kucheza
nchini kwao umeendelea, baada ya Simba sasa ni TP Mazembe ambao jana
mashabiki wa
klabu ya Al Merreikh ya Sudan wameufanyia fujo msafara wa klabu ya Tout
Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mjini
Khartoum, wakidai na wao walipokewa vibaya na klabu hiyo mjini
Lubumbashi wiki mbili zilikzopita.
Mazembe
yenye washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas
Emmanuel Ulimwengu ipo Khartoum kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi
ya Mabingwa Afrika dhidi ya Merreikh, hatua ya 16 Bora.
Katika
vurugu hizo, basi walilokuwa wamepanda wachezaji wa Mazembe limevunjwa
vioo na athari zaidi ikiwemo hali hali za wachezaji bado hazijajulikana.
Sasa
mechi hiyo iliyopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Omdurman, hatima yake
ipo mikononi mwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF)- ambayo inatarajiwa
kuchukua hatua muda mfupi ujao, kubwa zaidi ikitarajiwa kuifuta
mashindanoni Merreikh na kuifungia hivyo Mazembe kusonga mbele.
|
0 comments:
Post a Comment