Kim Poulsen ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania (Taifa Stars) kuanzia Mei 11 mwaka huu kuziba nafasi ya Jan Poulsen.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Rais wa TFF, Leodegar Tenga
amesema Kim amepewa mkataba wa mwaka mmoja baada ya Shirikisho kuamua
kutomuongezea mkataba Jan. Mkataba wa Jan uliokuwa wa miaka miwili
unamalizika Julai 30 mwaka huu.
Amesema
kwa vile Taifa Stars inakabiliwa na mechi za mchujo za Kombe la Dunia
raundi ya pili Kanda ya Afrika na mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya
Afrika (CAN), TFF imeona ni lazima iwe na kocha mpya mapema kabla ya
mkataba wa Jan kumalizika.
Kim
ambaye ni raia wa Denmark amekuwa nchini kwa mwaka mmoja sasa
akifundisha timu za Taifa za vijana wenye umri chini ya miaka 17
(Serengeti Boys) na miaka 20 (Ngorongoro Heroes), hivyo anawafahamu
vizuri wa wachezaji wa Tanzania.
TFF
imeanza mchakato wa kutafuta kocha mwingine wa timu za vijana
atakayeziba nafasi ya Kim. Ili kuwa na makocha wenye falsafa moja, kocha
huyo anatafutwa kutoka Denmark.
0 comments:
Post a Comment