skip to main |
skip to sidebar

5/13/2012 10:42:00 AM

Unknown
No comments

TIMU soka ya Wanawake ‘Twiga Stars’ imeendelea kufunzwa soka na wenzao
wa Zimbabwe baada ya leo kupokokea kichapo cha mabao 4-1 katika mchezo
wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam.
Mchezo huo ulikuwa ni maalum kwa kuzinoa timu hizo zinazojiwinda na
mechi zake za kuwania kucheza fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC)
ambapo Twiga itakwaana na Ethiopia Mei 26 mwaka huu huku Zimbabwe
itakipiga na Nigeria.
Kipigo cha Twiga dhidi ya Zimbabwe ni mara ya pili ambapo mara ya
kwanza ilikuwa nusu fainali ya Kombe la COSAFA ambapo katika mechi hiyo
iliyochezwa Julai 5 jijini Harare , Zimbabwe ilishinda kwa penalti 4-2.
Aidha, timu ambazo jana ilikuwa mara ya tatu kukutana, mara ya pili
walkikwaana kwenye michezo ya All Africa Games (AAG) iliyofanyika Maputo
, Msumbiji ambapo timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.
Katika mchezo wa jana, Rufaro Machungura aliiandikia Zimbabwe bao la
kwanza katika dakika ya 5 ya mchezo baada ya mabeki wa Twiga
kujichanganya.
Dakika ya 17 Nokuthula Ndolovu alimalizika kazi nzxuri ya washambuliai
wake kwenye eneo la hatari na kuandika bao la la pili ambalo lilidumu
hadi timu hizo zinakwenda mapumziko ambapo Zimbabwe ilikuwa ikiongoza
mabao 2-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kucheza kwa taratibu kabla ya
Asha Rashid kuiandikia Twiga bao lake pekee katika dakika ya 46
akimalizia kazi nzuri ya Mwanahamis Omari.
Zimbabwe ilitikisa nyavu za Twiga kwa mara ya tatu katika dakika ya 54
kupitia kwa Nokuthula alipotumia vema uzembe wa beki wa Twiga Fatma
Khatib aliyerkuwa katika harakati za kuokoa krosi yake.
Rufaro Machungura alifunga karamu ya mabao kwa Zimbabwe katika dakika ya
74 ambalo lililidumu hadi dakika 90 ya mchezo huo iliyomalizika kwa
Zimbambwe kushinda 4-1.
Aidha, mchezo huo ambao ulichelewa kupigwa kutoka na mvua iliyonyesha
jana jijini Dar es Salaam, Mwamuzi wa kimataifa JudithhGamba alimzawadia
kadi ya njano nyota wa Twiga Fatma Bashir kwa kumchezea vibaya Rufaro.
Katika mchezo huo Twiga ilifanya mabadiliko na kuwatoa Rukia Khamis,
Zena Khamis , Mwajuma Abdallah,na Fatma Hatib na kuwaingiza kuwaingiza
Fadhila Hamadi, Amina Ally, Siajab Hassan na Mwanaid Tamba.
Baada ya mchezo huo Twiga ambayo ilipata nafasi nyingi za wazi na
kushindwa kuzitumia walidai kufungwa kwao kulichangiwa na mvua
0 comments:
Post a Comment