WATU wanaosadikiwa kutumwa na wapinzani wa Mwenyekiti wa Yanga, Wakili
Lloyd Bahargu Nchunga wamevamia makao makuu ya klabu, kuvuruga Mkutano
wa Mwenyekiti huyo na Waandishi wa Habari mchana huu.
Watu hao wanadaiwa kufanya vurugu zilizosababisha uharibifu makao makuu
ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
Nchunga aliitisha mkutano na Waandishi wa Habari wa saa 5:00 asubuhi ya
leo, kuelelezea yale yaliyofikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji
jana.
0 comments:
Post a Comment